TIMU ya ES Setif ya Algeria imeondolewa
katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi, kufuatia vurugu
kubwa zilizofanywa na mashabiki wake katika mchezo na Mamelodi Sundowns ya
Afrika Kusini wiki iliyopita.
Taarifa ya Shirikisho la soka Afrika (CAF) imesema kwamba kufuatia tukio hilo
katika mchezo namba 98 wa 2016, amnao marefa walilazimika kuusitisha kabla ya
kumalizika, Setif imeadhibiwa.
Ripoti ya marefa imesema amani ilichafuka uwanjani baada ya mashabiki kurusha mioto, chupa na mawe na kusababisha watu kadhaa kujeruhiwa kabla ya walinzi kuingilia kati kutuliza hali hiyo.
Kwa sababu hiyo, kwa kutimia ibara ya saba ibara ya tatu ya kanuni za mashindano, Kamati ya Maandalizi ya michuano ya klabu ya CAF imeifuta ES Setif na hatua zaidi zitachukuliwa na Bodi ya Nidhamu ya shirikisho hilo.
Ibara ya saba kanuni ya tatu inasema: “3. Iwapo refa atalazimika kuvunja mchezo kabla ya kumalizika muda wa kawaida kwa sababu ya vurugu uwanjani, timu mwenyeji itapoteza mchezo na inaweza kuondolewa kwenye mashindano,”.
Na baada ya
maamuzi hayo ,Kundi B linabaki na timu tatu na Zamalek ndiyo inaongoza kwa
point 3 wakati Enyimba na Mamelodi hazina point.
No comments:
Post a Comment