MABINGWA WATETEZI wa UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Barcelona, ilitoka nyuma kwa Bao 1-0 na kuichapa Bayer Leverkusen 2-1 huku Bayern Munich wakiicharaza Dinamo Zagreb 5-0 lakini Klabu za England, Arsenal na Chelsea, zilifungwa Mechi zao za Makundi ya UCL.
Huko Nou Camp, Bayer Leverkusen walitangulia kwa Bao la Dakika ya 22 la Kyriakos Papadopoulos lakini Bao 2 ndani ya Dakika 2, Dakika ya 80 na 82, za Sergi Roberto na Luis Suarez ziliwapa Barcelona ushindi wao wa kwanza wa Kundi E baada ya kutoka 1-1 na AS Roma katika Mechi yao ya kwanza ya Kundi hili.Katika Mechi nyingine ya Kundi E, BATE Borisov iliitandika AS Roma 3-2.
Kwenye Kundi F, Bayern Munich ilipata ushindi wao wa pili mfululizo baada ya kuinyuka Dinamo Zagreb 5-0 huko Munich huku Arsenal ikipokea kichapo chao cha pili mfululizo, safari hii wakiwa kwao Emirates, walipotandikwa 3-2 na Olympiakos.
Bao za Bayern zilifungwa na Hetitriki ya Robert Lewandowski, Douglas Costa na Mario Gotze.Huko London, Felipe Pardo aliipa Olympiakos Bao la kuongoza lakini Theo Walcott akaisawazishia Arsenal ambao walikwenda Mapumziko wakiwa nyuma 2-1 baada ya Kipa wao David Ospina kujifunga mwenyewe.
Kipindi cha Pili, Arsenal walisawazisha Dakika ya 65 kwa Bao la Alexis Sanchez lakini Dakika 1 baadae Olympiakos walifunga Bao la 3 na la ushindi wa 3-2 kupitia Alfred Finnbogason.
Hii ni Mechi ya pili mfululizo kwa Arsenal kuchapwa katika Kundi F baada kupigwa 2-1 na Dinamo Zagreb na sasa wana kibarua kigumu cha kufuzu na kuwa Timu ya kwanza kufanya hivyo tangu Msimu wa 2012/13 tangu Galatasaray walipofungwa Mechi mbili za kwanza na kuweza kusonga hatua ya Mrtoano ya UCL.
Ili kufanya hivyo, Arsenal inabidi kwanza washinde Mechi zao mbili zinazokuja na zote ni dhidi ya Bayern Munich.Kwenye Kundi G, FC Porto, ikiwa kwao Ureno Estadio do Dragao Jijini Porto, iliicharaza Timu ya Mreno mwenzao Jose Mourinho, Chelsea, Bao 2-1.
Bao za Mechi hii zilifungwa na Andre Andre kwa FC Porto katika Dakika ya 39 na Chelsea kusawazisha Dakika ya 45 kwa Frikiki ya Willian.Kichwa cha Maicon katika Dakika ya 52 kiliwapa FC Porto ushindi wa Bao 2-1.
Katika Mechi nyingine ya Kundi hili la Chelsea, Dinamo Zagreb ilitamba Ugenini baada ya kuichapa Maccabi Tel Aviv 2-0.Leo Usiku zipo Mechi za pili za UCL kwa Timu za Makundi A hadi D.
MATOKEO:
Jumanne 29 Septemba 2015
KUNDI
E
Barcelona
2 Bayer Leverkusen 1
BATE
Borislov 3 AS Roma
2
KUNDI
F
Arsenal
2 Olympiakos
3
Bayern
Munich 5 Dinamo Zagreb 0
KUNDI
G
FC
Porto 2 Chelsea
1
Maccabi
Tel Aviv 0 Dynamo Kiev 2
KUNDI
H
Lyon
0 Valencia
1
Zenit
St Petersburg 2 KAA Gent 1
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RATIBA
Jumatano
30 Septemba 2015
KUNDI
A
Malmö
FF v Real
Madrid
Shakhtar
Donetsk v Paris St
Germaine
KUNDI
B
CSKA
v PSV
Man
United v VfL
Wolfsburg
KUNDI
C
1900
FC Astana v
Galatasaray
Atletico
Madrid v
Benfica
KUNDI
D
Borussia
Mönchengladbach v Man
City
Juventus
v
Sevilla
No comments:
Post a Comment