Wakulima
wa Kilimo cha Mbogamboga na Matunda wilayani Lushoto, mkoani hapa, wameoimba
Serikali kuwapunguzia gharama za pembejeo za kilimo ili walime kwa kufuata kanuni za kilimo cha kisasa.
Wakizungumza
hivi karibuni kwenye kikao cha Umoja wa Wakulima wa Mbogamboga na Matunda
Wilaya ya Lushoto na Korogwe ulioitishwa na Shirika la Oxfam Tanzania
tawi la Lushoto, wakulima hao wamesema kuwa kwa kipindi kirefu wameomba
Serikali kupunguza gharama bila ya mafanikio.
Wamesema
hali hiyo imekuwa ikirudisha nyuma jitihada zao, badala yake wameendelea kulima
kwa mazoea jambo ambalo linawafanya wengi kushindwa kupata faida stahiki ya
kilimo.
Mmoja
wa wakulima hao Bw,dhahabu amesema ni jambo la kushangaza kuona mkulima wa
Lushoto akiwa maskini ilhali wilaya hiyo ina rutuba inayofaa kwa aina
tofauti za kilimo, ikiwamo kilimo cha njegere, hivyo kuitaka
Serikali kuwaunga mkono kwa kuwapatia pembejeo.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Lushoto, Jumanne Shauri amelitaka
Shirika hilo kutoa elimu kwa wakulima kuhusu kilimo cha mbogamboga na matunda,
kwa sababu wengi hawana elimu hiyo.
No comments:
Post a Comment