HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Sunday, 2 February 2014

BREAKING NEWZZZZ** KOCHA WA MGAMBO SHOOTING,MOHAMMED KAMPIRA AACHIA NGAZI.


ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting yenye maskani yake Handeni Mkoani Tanga,Mohamed Kampira

oscar assenga,tanga.
ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa timu ya Mgambo Shooting yenye maskani yake Handeni Mkoani Tanga,Mohamed Kampira ameamua kujiuzulu nafasi ya  kuifudisha timu hiyo kwa  sababu ya kukosa ushirikiano wa kutosha na uongozi wa ngazi ya juu ya timu hiyo.

Kampira aliyesema hayo jana ambapo alisema kuwa ameachia ngazi kwa manufaa ya timu kwa sababu timu ni chombo cha watu na asingependa kuona timu hiyo haifanyi vizuri kwa sababu yake .

Alisema kitu kingine ni kutokana na matatizo yake ya kifamilia na kuhaidi kukabidhi barua ya kuachia ngazi kwenye timu hiyo kwa uongozi wa timu hiyo pindi timu hiyo  Jumatatu wakati timu itakaporudi kutoka jijini Dar es Salaam.

'Sababu kubwa ni kukosa ushirikiano kwani ni dhahiri kabisa unapokuwa mwalimu kwenye timu yoyote ile na ukashindwa kuelewana na uongozi hasa kwenye mambo muhimu hautaweza kuendelea kufanya kazi zaidi ya kuachia ngazi "Alisema Kampira.

Akizungumzia soka la Tanzania hasa kwa vilabu vinavyoshiriki Ligi kuu soka Tanzania bara,Kampira alisema mfumo walionao viongozi wa vilabu kuingilia maamuzi ya mabenchi ya ufundi utaua mpira wa Tanzania na kushindwa kupiga hatua.
Kikosi cha Mgambo Shooting

No comments:

Post a Comment