HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Tuesday, 21 January 2014

“TAZAMA KALI YA MWAKA TANGA” MWANAJESHI FEKI ATIWA MBARONI JIJINI AKITAKA KUFANYA UTAPELI KATIKA OFISI YA DC


Koplo Mponji akihojiwa na Waandishi wa Habari(Hawapo Pichani)


Hapa akijaribu kutoa maelezo yake yenye utata mwingi

Na Godwin Lyakurwa TANGA
Vikosi vya Ulinzi na Usalama Wilayani hapa vinamshikilia Edward John Mponji (31) kufuatia kwenda Ofisi ya Mkuu wa Wilaya  ya Tanga na kujitambilisha kuwa yeye ni Koplo wa Jeshi la Wananchi JWTZ akifanya mpango wa kijana wake aingizwe kweny jeshi la kujenga Taifa JKT.

Koplo “Mponji” alikwenda Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga Halima Dendego mnamo Januari siku ambayo kamati ya Ulinzi na Usalama wilayani hapa ilikuwa katika zoezi la kuwafanyia usaili vijana wanaotakiwa kuinguizwa kwenye mpango wa jeshi la kujenga Taifa.

Akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mponji alijitambulisha kuwa yeye ni afisa wa JWTZ ambaye kwa sasa yupo kikosi cha 36 KJ Mkoani Pwani ambapo aliambatana na Kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe Mpango ili apate nafasi.

Hata hivyo wakati akitoa maelezo hayo  Mshauri wa Mgambo wa Wilaya ya Tanga Sir Meja Albano Semfuko alimtilia shaka na kumjulisha Mkuu waWilaya ambaye aliamuru ashukiliwe kwa mahojiano zaidi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Wilaya alisema kuwa baada ya Mahojiano ilibainika kuwa Mponji si askari wa JWTZ na ndipo akapelekwa nyumbani kwake Mtaa wa Magomeni ambapo alikutwa na Sare za JWTZ zikiwa na Cheo Cha Koplo.

Alisema wakati akikamatwa Mponji alikuwa amevaa kaptula ya Jeshi la Polisi lakini alipowekwa Rumande katika kituo cha Polisi Chumbageni alifanya njama za kuivua na kumpa Mahabusu aliekuwa akitoka na kutoweka nayo.

Mponji alioneshwa kwa Waandishi wa Habari akiwa amevaa Sare za Jeshi la JWTZ ambapo alipohojiwa alishindwa kutoa maelezo ya kueleweka juu ya wapi alipozipata sare za Jeshi hilo ingawa alikiri kuwa aliwahi kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841 KJ Mafinga.

Kufuatia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Tanga Bi Halima Dendego aliamuru Jeshi la Wananchi kwa kushirikiana na Polisi kumfanyia uchunguzi wa kina ili kubaini Mtandao wake.

Koplo Mponji akitoa maelezo kwa Wanausalama

No comments:

Post a Comment