Na
Elizabeth Kilindi,Tanga.
HALMASHAURI
ya Jiji la Tanga imekusudia kutumia zaidi ya tsh billion 61.1 kwa
ajili ya uendeshaji wa miradi mbalimbali ya Jiji
hilo na utoaji wa huduma kwa wananchi katika kipindi cha mwaka wa fedha
2014/2015.
Hayo yalielezwa na meya wa Jiji la Tanga, Omari Gulled wakati akitoa taarifa kwa wananchi kuhusiana na mchakato wa bajeti ya halmashauri hiyo na mipango iliyopo ya uendeshaji wa shughuli za maendeleo kwa wananchi wake.
Gulled alisema kuwa bajeti hiyo imekamilika baada ya taratibu zote kufuatwa ikiwemo michakato ya kamati mbalimbali na kwamba kamati hizo zimehitimisha kazi zake mapema ya January 11 ya mwaka huu.
Hata hivyo meya huyo alifafanua kuwa katika bajeti hiyo mapato ya ndani yanatarajiwa kufikia tsh billion 7.7 ambapo tsh million 380 kati ya hizo ni ruzuku kutoka serikalini,wahisani na michango ya wananchi.
Alieleza kuwa tsh billion 13 ni fedha zinazotarajiwa kupatikana kwa kutokana na mradi unaofadhiliwa na benk ya dunia kwa ajili ya kurahisisha utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo na huduma za kijamii.
“Miradi mikubwa tuliyonayo ni barabara,ujenzi wa kituo kipya cha mabasi ya mikoani kinachojengwa Kange……..haya yote ni utekelezaji wa mwaka 2014/2015 kulingana na upatikanaji wa fedha tarajiwa” alisema Gulled.
Aidha aliitaja miradi midogo ya ndani inayotarajiwa kutekelezwa katika Jiji hilo kwa kipindi hicho kuwa ni ujenzi wa maabara kwa kila sekondari ya Kata, madawati, ukarabati wa barabara za Jiji, vituo vya afya, ujenzi wa hospitali ya Wilaya, mradi wa maji na umeme.

No comments:
Post a Comment