HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA

HII NI KWA MARA YA KWANZA JIJINI TANGA
Tangaza biashara yako sasa uwafikie wateja wako kwa haraka na kwa gharama nafuu kupitia mfumo wa kisasa wa Digital Display Advertisement. Kupitia mfumo huu wateja wako watapata fursa ya kuona huduma zako na taarifa zote muhimu kupitia luninga kuwa za kisasa.

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA

KIJIWE KIPYA CHA BURUDANI JIJINI TANGA
MPANGO MZIMA WA KULA BATA UKO HAPA

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...

....HABARI NJEMA KWA AFYA YAKO...
.....tumia fursa yako vizuri....

Thursday, 17 May 2018

SUGU AELEZA YALIYOMKUTA AKIWA JELA.



Mbunge wa Mbeya kupitia CHADEMA Joseph Mbilinyi maarufu kwa jina la Sugu, amesema alishangazwa na kitendo cha kusikia imepigwa simu kutoka juu, na kueleza kwamba ni lazima yeye na Masonga wavae sare za jela

Akizungumzia suala hilo Sugu amesema kwamba kitendo hicho kilimshangaza kwani kulikuwa kuna watu wengine wengi walikuwa hawana sare na wamefungwa mule muda mrefu lakini walikosa sare, hivyo kitendo cha kulazimishwa yeye ambaye yuko kwa muda mfupi kilikuwa kinamshangaza.

“ Nisiite kujisikia vibaya niite kushangaa, ni siku ambayo maagizo kutoka juu, ilipigwa simu kwamba lazima Sugu avae uniform na Masonga, unaweza ukaona kwamba zaidi ya wafungwa 600 hawana uniform, Sugu yuko pale mmemfunga kwa miezi mitano, anatakiwa kutumikia kama miezi mitatu, lakini unamlazimisha avae uniform, lakini kuna wafungwa pale wamefungwa maisha mamia kwa mamia hawana uniform, kwa nini usiangalie namna ya kuwapatia wale uniform unahangaika na mtu ambaye anapita tu!?”, amesema Sugu.

Sugu ameendelea kwa kusema kwamba kitendo cha yeye kulazimishwa kuvaa sare hakikumkwaza kwani aliona inamsaidia kuhifadhi nguo zake.

“Zilitafutwa siku hiyo hiyo uniform, wakaja wakatuletea uniform ambazo zimevaliwa tukagoma, tukakataa kwa sababu hatuwezi kuvaa nguo ambazo hatujui zimevaliwa na nani, wakaenda kuhangaika kila kona sijui walitoa Segerea, lakini walitumia nguvu kuhakikisha wanatuvalisha uniform, wao walidhani wakimvalisha Sugu uniform ataathirika kisaikolojia, lakini we umeshanifunga kuvaa nguo ni kitu gani, kwanza utanisaidia kutunza nguo zangu", amesema Sugu.

Sugu aliachiwa huru mapema wiki iliyopita kwa msamaha wa Rais baada ya kutumikia kwa muda mfupi kifungo chake cha miezi mitano katika gereza la Ruanda mkoani Mbeya, akiwa na mwenzake Emmanuel Masonga

Monday, 7 May 2018

MBOWE ATOA KAULI KUFUATIA MADIWANI 46 WA CHADEMA KUHAMIA CCM

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (CHADEMA) Mhe, Freeman Mbowe amefunguka na kutoa neno kuhusu madiwani 46 ambao wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kusema kuwa jambo hilo linafanywa na CCM kwa lengo la kuwakatisha tamaa wana CHADEMA.

Mbowe amesema kuwa wapo watu wanadhani kitendo cha baadhi ya madiwani kuhama CHADEMA na kwenda CCM ni kukiuwa chama hicho na kusema suala hilo haliwezi kutokea kwani madiwani wa CHADEMA nchi nzima wapo zaidi ya 1130 huku madiwani 46 ndiyo waliohama na kwenda CCM na kusema kitendo hicho kinawapa funzo katika maandalizi ya kutafuta viongozi ambao kweli wanaweza kukisimamia chama na si wale wanaotafuta fursa za kutoka kupitia uongozi.

"Kazi kubwa inayofanywa na CCM ni kuwakatisha tamaa na jambo ambalo limefanyika karibuni ambalo linaonekana wana CHADEMA wengi wamerudishwa nyuma basi ni suala la madiwani, madiwani wamenunuliwa jamanii wanaunga mkono juhudi, kuna watu wengine ni mizigo lakini sasa tunafanyaje lakini watu wa CHADEMA wanakata tamaa eti madiwani wanaisha chama kinakufa, hiki chama hakifi mzee CHADEMA nchi nzima ina madiwani 1184 madiwani mpaka dakika hii wameondoka ni madiwani 46 kwa hiyo tuna madiwani zaidi ya 1130 wamebaki CHADEMA halafu mtu anasema CHADEMA inakufa una akili wewe?

Aidha Mbowe amesema kuwa hao viongozi ambao wanahama kutoka CHADEMA na kwenda CCM kwao ni kama funzo kwamba wapo viongozi na watu mbalimbali ambao wapo ndani ya CHADEMA kwa lengo la kutafuta fursa tu na wanapoikosa hiyo fursa na ulaji wanaamua kuondoka.

"Kwetu ni funzo tunapojiandaa kwenda kwenye uchaguzi wa Wenyeviti wa Mtaa, Vijiji, madiwani, wabunge hata nafasi ya Urais tukajiandaa na kina nani wanaoishi ndoto ya CHADEMA lazima safari hii tujiridhishe mapema huyu tukimpa nafasi basi historia yake tunaijua vyema" alisema Mbowe

SERIKALI HAIJAZUIA HARAKATI ZA KISIASA: NAIBU WAZIRI MAVUNDE.

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde,imesema kwamba haijaweka zuio kwa vyama vya siasa kufanya siasa, bali kuna sheria ambazo zinapelekea kutokea kwa hali hiyo.

Akijibu swali Bungeni kwa niaba ya Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde, amesema seikali haijuzia vyama vya siasa kufanya siasa, kwani imevipa uhuru vyama hivyo kufanya shughuli zake za kisiasa, isipokuwa kuna sheria za jeshi la polisi ndizo zinatoa muongozo juu ya ufanyikaji wa mikutano ya siasa na maandamano.

“"Si kweli kwamba serikali inazuia harakati za kisiasa, sheria imetoa uhuru kwa vyama kutafuta wanachama na kufanya mikutano lakini iko subject na sheria nyinginezo, ikiwemo sheria ya Police force na auxiliary service act ambayo pia imeweka masharti katika section namba 44 na 45 ya namna vyama vya siasa vinaweza vikafanya kazi zao hasa katika mikutano na maandamano mbali mbali”, amesema Anthony Mavunde.

Swali lililojibiwa lililoulizwa na Mbunge wa Rombo Joseph Selasini ambalo lilitaka serikali kusimamia sheria ikiwemo inayowaruhusu wanasiasa kufanya siasa.

RAIS MAGUFULI AONYA MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI MOROGORO.

Rais Magufuli amewataka Wakulima na Wafugaji kuacha vitendo vya kupigana na kwamba katika serikali yake hakuna mtu aliyeko juu zaidi ya mwingine na kusisitiza kwamba watanzania wote ni sawa kwani ndiyo waliyomchagua.

Akizungumza jana na wananchi wa Morogoro akiwa njiani kuelekea Msamvu Raid Magufuli alisema kwamba kamwe vitendo vya kupigana visirudie katika serikali yake na kwamba wale watakaokiuka watashughulikiwa.

Aidha aliongeza kuwa anataka wakulima na wafugaji waishi kwa kuheshimiana kwani yeye anachokihitaji ni amani.

Pamoja na hayo, Rais Magufuli amewashangaa Wafugaji kuwalisha ng'ombe mazao ya wakulima ilhali kuna majani ya kutosha na wanaposhtakiwa wanaamua kutumia gharama kubwa kuhonga hata kufikia hatua ya kuuza ng'ombe.

"Mimi nimekaa kwa wamasai Monduli, nimechunga mpaka ng'ombe za wamasai nikiwa JKT Makuyuni. Ni watu wazuri tu. Sasa kwanini wamasai wa huku wanachukia mali za wengine wakulima? Nataka niwaaeleze nitalifuatilia hili.

Pamoja na hayo aliongeza "Kama yupo mmoja ambaye analiisha kila siku anajifanya ana mali huyo mimi ndiye ntalala naye mbele mwenyewe".
Picha na Maktaba..

KUPANDA KWA BEI YA MAFUTA YA KULA...WABUNGE WAIBANA SERIKALI

Wabunge wa CCM, Juma Nkamia (Chemba) na Hussein Bashe (Nzega Mjini), wameibana Serikali wakitaka ishughulikie kupanda kwa bei ya mafuta na kuondoa kodi ya tende ili kuwapunguzia mzigo wa gharama waislamu katika mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Hayo yamejiri leo Mei 7, 2018 bungeni mjini  Dodoma, wakati Nkamia aliposimama kuomba mwongozo kuhusu  mafuta na Bashe kutaka kuahirishwa kwa shughuli za Bunge kwa dakika 30 ili kujadili suala la kodi ya tende ili iondolewe kama ilivyo kwa nchi jirani.

Nkamia alikuwa wa kwanza kuzungumza akisema, kubainisha kuwa katika baadhi ya vyombo vya habari kuna taarifa za kuadimika kwa mafuta ya kula, “hali hii inasababisha  mafuta kupanda bei kwa haraka, Serikali inatoa kauli gani ili kuwaondolewa wananchi hofu.”

Kwa upande wake Bashe akitumia kanuni ya 69 ya kuahirisha shughuli za Bunge, amesema, “mwezi wa Ramadhani unakaribia na kama alivyosema Nkamia, bei ya mafuta imepanda, sukari imepanda, lakini nchi zinazotuzunguka zimefuta kodi za tende.”

Akijibu mwongozo huo, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema tatizo lililojitokeza ni suala la kodi kwani kwa sasa Taifa lina hifadhi ya mafuta ghafi tani 40,000 na meli zilizopo nje zina tani 50,000.

“Jumla zilizoko nje na ndani  zina tani 90,000. Kinachoweka tatizo ni kodi kwa sheria tulizopitisha Tanzania, tunatoza kodi (meli kutoka nje ya nchi) asilimia 10 kwa mafuta ghafi,” amesema.

“Ila kwa vipimo vinaonyesha si mafuta ghafi ni mafuta masafi hivyo wanataka kutoza asilimia 25 na hapo ndipo kuna tatizo la hadi kufikia leo au kesho tutatoa majibu ya tulipofikia.”

Kuhusu hoja ya tende iliyoulizwa na Bashe, Waziri Mwijage amesema, “ni suala la kwenda kuzungumza na waziri wa fedha, tutalipeleka kuweza kumshawishi ili Bunge na nchi ichume thamani.”

Naye, Waziri wa Kilimo, Dk Charles Tizeba amesema suala la mbegu za pamba kutumika kukamulia mafuta zilipatikana mwaka jana zaidi ya laki moja.

“Suala la mafuta yanayotokana na pamba, kwa uhakika hayakutarajia kuwa mengi, sasa Serikali inachokifanya inaagiza kutoka nje, niseme tu suala la mafuta linafahamika na Serikali inalifanyia kazi na haitapanda bei sana kama mbunge (Nkamia) alivyoonyesha wasiwasi,” amesema Tizeba.

Friday, 27 April 2018

HABARI NJEMA KWA WAKULIMA NA WAFUGAJI JIJINI TANGA.


MBUNGE LEMA AKAMATWA NA POLISI MKOANI ARUSHA KWA UCHOCHEZI.



Mbunge wa Arusha Mjini Mhe. Godbless Lema leo April 27, 2018 amekamatwa na polisi na kufunguliwa kesi mpya kuhusu uchochezi kwa ndoto aliyowahi kuota kuhusu Rais Dkt. John Pombe Magufuli miaka miwili iliyopita.
Mkurugenzi wa Itikadi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema amethibitisha hilo na kusema kuwa Lema leo alihudhuria Mahakamani kwa ajili ya kesi iliyokuwa ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka miwili iliyopita.

"Jeshi la Polisi Mkoani Arusha limemkamata Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kwa kile kinachodaiwa "uchochezi". Dhidi ya Mh Rais kuhusiana na ndoto aliyowahi kuota. Lema alihudhuria Mahakamani siku ya leo kwa ajili ya kesi iliyokua ikimkabili kuhusiana na ndoto alizoota miaka 2 iliyopita. Baada ya Mahakama kufuta kesi hiyo leo na kuachiwa...Polisi walimkamata tena na kumfungulia kesi upya kwa mashtaka yale yale" alisema John Mrema

Kesi hii ni mwendelezo wa kesi iliyokua ikimkabili Mh Godbless Lema na ambayo ilimsotesha Mahabusu (Magereza) kwa zaidi ya miezi 4 mwaka juzi kabla ya kuachiwa kwa dhamana mapema mwaka jana.