TIMU ya soka Coastal Union ya Tanga
inatarajia kusheherekea miaka hamsini na nne ya Uhuru wa Tanzania kwa kucheza
mechi ya kirafiki na timu ya AFC ya Arusha itakayochezwa kwenye uwanja wa CCM
Mkwakwani Desemba 9 mwaka huu.
Mechi hiyo ni maandalizi kwa timu
hiyo kujiandaa na mechi zake za Ligi kuu soka Tanzania bara baada ya mapumziko
ya siku kumi kutokana na Ligi kuu kusimama kwa muda ambapo itaendelea Desemba
26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa
habari leo,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema kuwa mechi hiyo
itakuwa ni muhimu kwa timu hiyo kujitayarisha kwa ajili ya raundi inayofuata
kwenye michuano hiyo.
Amesema kuwa baada ya kumalizika
mechi hiyo wataangalia uwezekano wa kutafuta mechi nyengine ya majaribio kabla
ya kuanza ligi hiyo ambayo msimu huu imeonekana kuwa na upinzani mkubwa
Aidha amesema kuwa timu hiyo ya
AFC yenye makazi yake Mkoani Arusha inatajiwa kuwasili mkoani Tanga Desemba 8
mwaka huu kwa ajili ya mtanange huo lengo likuwa kuziandaa timu zote mbili kwa
mashindano yanayowakabili.
Amesema kuwa mechi hiyo ina
umuhimu kwa timu zote mbili sisi ni kujiandaa na Michuano ya Ligi kuu Tanzania
bara raundi inayofuata na wapinzania wetu wanajiandaa na Ligi daraja la
kwanza hapa nchini.
Hata hivyo amesema kuwa mazoezi
ya timu hiyo yameendelea kushika kasi kwenye viwanja vya Mkwakwani mjini Tanga
baada ya wachezaji wote waliokwenda mapumziko kurejea kwa asilimia kubwa.

No comments:
Post a Comment